Tuesday, April 6, 2021

Rais Samia Suluhu aagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Habari kuwafungulia Vyombo vya Habari kama TV zilizofungiwa ila wafuate Sheria.


Pia, ametaka Kanuni ziweke wazi makosa na adhabu zake ili kusiwe na ubabe kwa kuwa Serikali inaamini katika Uhuru wa Vyombo vya Habari.


Aidha, ametaka Wasanii waangaliwe kwa umakini ili kukuza vipaji vinavyoibuka kila siku pamoja na kutunza tamaduni na silika ya Tanzania japo hatuna tamaduni moja.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...