Sunday, April 11, 2021

Njombe:Vijana waliojiajiri kwenye kilimo cha Nyanya wavuna mamiloni ya fedha

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Vijana na wakazi wa kijiji cha Matembwe wilayani Njombe wanaojishughulisha na kilimo pamoja na biashara ya nyanya wilayani humo,wametoa wito kwa vijana nchini kujishughulisha na kilimo ili kuepukana na changamoto kubwa ya ajira  inayoikabili taifa.


Vijana hao akiwemo Joseph Kabelege na Jastine Malekela wametoa wito huo walipotembelewa na mwandishi wetu katika shamba lao la nyanya lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja na kutegemewa na wakazi wa kata na kijiji hicho pamoja na wilaya kwa ujumla huku wakifanikiwa kiuchumi kutokana na kupata fedha mara baada ya mavuno ya Nyanya katika shamba lao.


"Ifike wakati sasa vijana tufunguke tuache kukaa na kuipigia kelele serikali haitoi ajira,hakuna serikali inayoweza kumaliza kutoa ajira kwa watu wote ni lazima tuthubutu hata kwenye kilimo"alisema Kabelege


"Kwenye hii ekari moja na robo nimepanda miche 6500 na kwa shina moja nilishafanya mahesabu kutoka linapoanza mpaka linapomalizia linaota matundu sio chini ya 100 au 120 na sio chini ya debe moja kwa mche mmoja na toaka nilipoanza kuvuna mpaka hapa leo wastani kwa debe moja nimekuwa nikuza kwa shilingi elfu kumi 10,000/="aliongeza Kabelege


Ezekiel Mwansopo ni mshauri wa maswala ya kilimo anyefanya kazi na kampuni ya Namaingo ni miongoni mwa vijana waliotembelea katika shamba la nyanya linalolimwa na vijana hao wa kijiji cha Matembwe.amesema licha ya kilimo kuwa na changamoto lakini anashukuru kuona vijana wameanza kufuata fursa katika kilimo.


"Tumeona hapa kijana analima na anaweza akapata debe moja katika mche mmoja na debe linauzwa shilingi elfu kumi kwa sasa na ana miche karibu 6500 ni kiasi gani cha fedha anachokizalisha lakini wengine unaona wapo huko mitaani wanasema wanahangaika na ajira wakati hapa wamejiajiri na wanapata pesa, niwasahuri vijana waweze kujituma kwenye kazi kama hii na ukiangalia Kabelege anaamua nizashile milioni ngapi kwa muda gani"alisema Ezekiel Mwansopo


Kwa upande wake Lusiana Nchine afisa kilimo na mifugo wa kijiji cha Matembwe amewataka vijana kuiga mfano wa wachache wanaojishugulisha na kilimo ikiwemo kilimo caha Nyanya katika kijiji hicho kwa kuwa ni kilimo cha muda mfupi lakini zao lake limekuwa na soko katika jamii.


"Fursa za kilimo zipo nyingi ni kiasi tu cha mtu kukaa na kutazama kipi kinaweza kunilipa kwa hiyo hata vijana wengine wanaweza wakaangalia huyu anaendesha maisha yake kwa kilimo cha nyanya je mimi naweza nikafanya kipi kwasababu hata kufuga nako ni kilimo nah ii tutaondokana na changamoto ya ajira"alisema Lusiana Nchine


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...