MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Leo Aprili 11,2021 amelezea alivyosikitishwa na msiba wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk. John Pombe Magufuli.
"Ni katika kipindi hiki ndugu zangu Watanzania Taifa letu lilikumbwa na taharuki kubwa tulimpoteza Rais wa nchi yetu Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli, nasikitika binafsi nilishindwa kurejea nchini kwa wakati kushirikiana na Watanzania wenzangu na viongozi wa nchi na Jumuiya mbalimbali za kimataifa katika kumsindikiza katika safari yake ya mwisho"
"Natoa pole nyingi kwa mama mjane Mama Magufuli, watoto, familia, ndugu na jamaa, Rais na mama yetu Samia Suluhu Hassan na chama chake Chama cha Mapinduzi, hakika ni mwisho wa zama Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe" –Freeman Mbowe.