Saturday, April 10, 2021

Mwanafunzi auawa kwa madai ya kuiba elfu 12






 Jeshi la polisi mkoani geita linamtafuta kijana anayefahamika KWA JINA la HAMADI JUMA MKazi wa mtaa wa nyanza kata ya kalangalala wilayani geita kwa tuhuma za kumuua methodi hasani mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa la saba aliyekuwa anasoma katika shule ya msingi kalangalala mkoani humo kwa kumshambulia na vitu vya ncha kali pamoja kumpiga mateke ngumi kwa madai kuwa mwanafunzi huyo amemuibia kiasi cha shilling eif 12 dukani kwake
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa geita ACP HENREY MWAIBAMBE amesema ni kosa kisheria kujichukua hatua mkononi na jeshi la polisi linafanya kila liwezekanalo kuhakikisha linamtia mbaroni kijana huyu aliyefanya mauaji hayo

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...