Leeds United wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu huu. (90min)
Hatima ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe katika klabu ya Paris St-Germain haijulikani baada ya nyota huyo aliye na umri wa miaka 22- kukataa kusaini mkataba mpya. (Telegraph – subscription required)Mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero
Mbappe hatasaini mkataba mpya PSG kwasababu anataka kujiunga na Real Madrid. (Cuatro – in Spanish)
Real Madrid wanajiandaa kumtumia mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, 20, katika mkataba wa kumsaini Mbappe msimu huu wa joto. (El Chiringuito, via Metro)
Winga wa Real aliye na umri wa miaka 29- Mhispania Lucas Vazquez, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, hajaamua kuhamia Bernabeu licha ya Manchester United na Chelsea kuonesha nia ya kutaka kumnunua. (Sun)
Chelsea inapania kuwasajili washambuliaji Erling Braut Haaland, 20, wa Borussia Dortmund na Aguero wa Manchester City msimu huu wa joto. (90min)Kylian Mbappe hatasaini mkataba mpya PSG kwasababu anataka kujiunga na Real Madrid
Lyon wameweka euro milioni 25 kama bei ya awali ya mchezaji wa Uswidi wa safu ya kati na nyuma Joachim Andersen, 24, ambaye yuko Fulham kwa mkopo. Manchester United na Tottenham pia zinamnyatia. (Metro)
Winga wa Japan Takumi Minamino, 26, anasema "alishangazwa" na uamuzi wa Liverpool kumtoa kwa mkopo kwenda Southampton mwezi Januari. (Independent)
Saints wanajadiliana kurefusha mkataba wa mshambuliaji wa Uingereza Theo Walcott katika uwanja wa St Mary's. Mchezaji huyo mwenye miaka 32- kwa sasa yuko kwa mkopo wa msimu mzima Everton. (Southern Echo)Lucas Vazquez hajaamua kuhamia Bernabeu licha ya Manchester United na Chelsea kuonesha nia ya kutaka kumnunua
Liverpool wamemchagua kiungo wa kati wa AZ Alkmaar Mholanzi Teun Koopmeiners,23, kujaza pengo litakaloachwa na Georginio Wijnaldum, 30. (AS – in Spanish)