Friday, April 9, 2021

CAG: Stendi ya Magufuli itasababisha foleni barabara ya Morogoro



Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imesema ujenzi wa kituo cha mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi mkoani Dar es Salaam haukujumuishwa katika upanuzi wa barabara kutoka Kimara kwenda Kibaha mkoani Pwani.
"Kulingana na mahojiano na maafisa wa Wakala wa Barabara (TANROADS) na jinsi tulivyoona kwenye eneo la mradi, nilibaini kuwa mradi wa upanuzi barabara ya Morogoro haupo kwenye mwelekeo wa kufikia malengo yake ya kupunguza msongamano wa vyombo vya usafiri kutokana na ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Mwisho." CAG

"Ujenzi huu ulianzishwa wakati mradi wa upanuzi unaendelea. Kwa hivyo, kituo cha mabasi hakikujumuishwa katika mpango na usanifu wa mradi huu. Zaidi ya hayo, uendeshaji wa kituo cha mabasi mbali na kusababisha msongamano wa magari unaweza kusababisha changamoto zaidi kwenye makutano yanayoingia barabara ya Morogoro. Kituo hiki cha mabasi kinatarajiwa kuhudumia mabasi 700 kila siku," CAG

"Mipango hii miwili ilifanywa bila ushirikiano kati ya taasisi hizi za serikali. Ukosefu wa mpango mkuu jumuishi wa kisekta baina ya taasisi za umma ndio chanzo kikuu cha tatizo hili," CAG

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...