Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwa akaunti ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ilitumika kupitisha malipo batili ya Sh261 milioni.
Akiwasilisha ripoti hiyo mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 CAG, Charles Kichere amesema, "nilibaini milioni 261.35 zikiwekwa katika akaunti ya Jeshi la Zimamoto, katika moja ya benki ya biashara kwa kipindi tofauti hata hivyo uongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hazikutambua chanzo vya fedha hizo na hazikuwa na mawasiliano yaliyofanyika na benki kuhusiana na mapokezi ya fedha hizo."
"Pia nilibaini kiasi cha fedha kilichukuliwa na mtunza fedha wa Zimamoto na uokoaji kutoka kwenye akaunti hiyo kwa kipindi tofauti kwa kutumia nyaraka za kughushi."