Thursday, March 18, 2021

Wanawake wa China wana akiba kubwa ya fedha kuliko Wanaume



Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Fedha ya Jumuishi ya China International Forum for China Financial Inclusion imeonesha kuwa, kutokana na wastani wa thamani unaolinganishwa kati ya wanawake na ule wa wanaume, alama za jumla za uwezo wa kifedha wa wanawake ni wa juu zaidi.


Wanawake wameonekana kuwa ni hodari zaidi kuliko wanaume kwenye usimamizi wa matumizi ya fedha wakati wa siku za kawaida, huku wanaume wakionesha uhodari zaidi kuliko wanawake katika uwekezaji katika siku zijazo.


Utafiti kuhusu uwekezaji na usimamizi wa fedha wa wanawake duniani, pia umeonesha kuwa kati ya masoko yote yaliyohusishwa katika utafiti huo, China ni sehemu ya kipekee ambayo wanawake wana akiba kubwa zaidi ya fedha kuliko wanaume, na asilimia 73 ya wanawake wa China wanashughulikia mpango wa fedha na uwekezaji.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...