Monday, March 15, 2021

Simba Kupewa Pointi 3 za Al Merrikh Ipo Hivi




BAADA ya uongozi wa Simba kupitia kwa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kuandika barua kwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuomba ufafanuzi juu ya wachezaji wawili wa Al Merrikh waliocheza mchezo dhidi yao wakiwa wamefungiwa imeelezwa kuwa majibu yametolewa kwamba wachezaji hao hawana makosa.

 

Wachezaji hao wawili ambao ni Ramadhan Agab na Bakhit Khamis walicheza Machi 6, Uwanja wa Al Hilal kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi na ulikamilika kwa sare ya bila kufungana.

 

 

Habari zillieleza kuwa wachezaji hao wawili walikuwa wamefungiwa kucheza kwa kuwa kulikuwa na makosa kwenye mikataba yao jambo ambalo liliwafanya Simba kuhitaji ufafanuzi kutoka Caf.

 

 

Endapo ingebainika kwamba wachezaji hao walicheza kwa makosa kwenye mchezo huo basi Simba ingepewa pointi tatu za mezani na kuifanya ifikishe pointi 9 kwa kuwa ilikuwa ina pointi sita kabla ya kucheza nao na wakati huu ina pointi 7.

 

 

Taarifa zimeeleza kuwa Caf wamewaambia Simba kwamba wachezaji hao walikuwa wamefungiwa kucheza ligi ya Sudan lakini wanaweza kucheza mashindano yanayosimamiwa na Caf.

 

 

Hivyo kwa taarifa hiyo ni kwamba kesho wachezaji hao watakuwa sehemu ya kikosi kitakachomenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu na Simba haitapata pointi tatu.

 

 

Al Merrikh ikiwa kundi A inaonekana inaweza kuwa kikwazo kwa Simba kesho kwa kuwa ina pointi moja na kundi lipo wazi ikiwa itashinda kesho itafufua matumaini ya kufuzu robo fainali.

 

 

Pia ilifanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi jambo linalowafanya waje na mbinu mpya kusaka ushindi hivyo lazima Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kujipanga kusaka pointi tatu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...