Friday, March 19, 2021

Picha : WAJUMBE WA KAMATI YA AMANI MKOA WA SHINYANGA WASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA DK. MAGUFULI....'AMEACHA ALAMA KWA TAIFA'


Mwenyekiti wa  Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga wametia Saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi.

Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga wamesaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Machi 19,2021 katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Sheikh Balilusa Khamis na Katibu wa kamati Askofu Raphael Machimu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga.

Mbali na kusaini kitabu cha Maombolezo, Wajumbe hao wa kamati ya amani mkoa wa Shinyanga pia wamefanya dua/maombi kumuombea Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitoa salamu za rambirambi, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis amesema taarifa za kifo cha Dkt. Magufuli zimewasononesha sana na kwamba taifa la Tanzania limepoteza mtu muhimu aliyeiletea heshima kubwa nchi ya Tanzania na katika kuwapigania haki ya watu wanyonge.

Naye Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Askofu Raphael Machimu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga amesema Watanzania watamkumbuka Dkt. Magufuli kutokana na kwamba aligusa maisha ya kila mtu na kila mahali.

"Magufuli aligusa kila mahali akitetea wanyonge na kwa kweli ameacha alama kubwa katika taifa hili",amesema Askofu Machimu.

Aidha Askofu Machimu amewaomba Watanzania kuendelea kudumisha utulivu na amani ya nchi akibainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa pamoja na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli hivyo taifa halitatetereka na kwamba amani na mshikamano wa taifa utaendelea kuwepo.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Albert Msovela amesema serikali ya mkoa wa Shinyanga imeandaa Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ambapo Viongozi na wananchi wa mkoa wa Shinyanga watafika katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kusaini na kutoa salamu za rambirambi katika kipindi chote cha siku 21 za maombolezo ya kifo cha Dk. Magufuli.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Kulia ni Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga wakiwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Albert Msovela. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi na kutia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Albert Msovela akielezea kuhusu eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi na kutia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis (wa pili kushoto) akizungumza wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika eneo maalumu lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya Viongozi na Wananchi kutoa pole na salamu za rambirambi na kutia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Askofu Raphael Machimu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga akimuombea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Shinyanga, Sheikh  Soud Kategile ambaye ni Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga akimuombea dua aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Mwenyekiti wa  Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Askofu Raphael Machimu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Askofu Raphael Machimu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Shinyanga, Sheikh  Soud Kategile ambaye ni Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga  akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Shinyanga,akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , Albert Msovela akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , Albert Msovela akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mwenyekiti wa  Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akizungumza baada ya kusaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Askofu Raphael Machimu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga akizungumza baada ya kusaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mwenyekiti wa  Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Sheikh Balilusa Khamis akiteta jambo na wajumbe wa kamati hiyo baada ya kusaini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi mbalimbali wakiendelea kutia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog / Mwandishi wa Habari Kadama Malunde akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwandishi wa habari wa ITV , Frank Mshana akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera Amos John 'Mc Mzungu Mweusi' akitia saini Kitabu cha Kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...