Saturday, February 6, 2021

Wazazi, Chanzo cha Watoto Kukosa Ubunifu

  


Ubunifu kwa watoto umeelezwa kukwamishwa na mambo matatu  ikiwemo  adhabu wanazopewa watoto mara kwa mara.

 


Akizungumza katika Kipindi cha Mamamia cha East Africa Radio Msaikolojia John Lyadunda amesema wazazi wengi huadhibu watoto mara kwa mara wakijuwa kwa kufanya hivyo wanawajenga ilihali wanawaharibu kwa kuwajengea hofu katika kujaribu mambo mabalimbali.


"Ubunifu wa mtoto unajengwa tangu mtoto akiwa mdogo, adhabu za mara kwa mara zinaua ubunifu wa mtoto, ili mtu awe na hali ya ubunifu lazima afanye makosa ya mara kwamara ili aweze kujitafuta na afanye kitu kitakachoonekana" amesema Lyadunda.


Pia ameongeza kuwa Katika malezi mtoto anapokuwa haaminika katika kila kitu anachofanya kinau uwezo wa mtoto  kujiamini katika mambo mbalimabali ili kumjenge uwezo wa kukomaa katika mambo anayoweza kufanya.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

"mtoto anapokuwa haaminiki kwenye kila kitu anachofanya akinauua confidence yake, wazazi na walezi tumuamini mtoto kwa yale anayoyafanya atakama ni ya watoto" amesema Lyadunda

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...