Sunday, February 7, 2021

Wanakijiji wapokea taarifa walizozikataa msimu uliopita

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa kijiji cha Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe wamezipokea taarifa za mapato na matumizi za Desemba 2019 - Julai 2020 na ile ya Agosti 2020 - Desemba 2020 ambazo walikataa kuzipokea katika mkutano wa hadhara wa kijiji uliopita.


Licha ya wananchi hao kuzipokea taarifa hizo wamepata wasaa wa kuhoji mambo mbalimbali yaliyojitokea  kwenye taarifa hizo ikiwemo matumizi ya fedha za kijiji kuelekezwa zaidi kwenye posho za wajumbe jambo ambalo wamesema linakwamisha jitihada za kijiji hicho kupiga hatua Joyce Nyasanga, Zakayo Mahenge, Samson Rashid 


"Inaonekana wakati mwingine inaonekana mnaangalia kuwa kwa sasa tumeishiwa hapa tuende sasa kuchukua posho huko vijiji,mimi ni bora mkaniambia kwetua hapa habari ya hela sitaki"Alisema Joyce Nyasanga


Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Februari 04, 2021 Wananchi hao wamefika mbali zaidi na kueleza kutokuwa na imani na serikali ya kijiji hicho wakiituhumu kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo


"Tunaomba muongozo wenu kwamba sasa tunatoka na lipi kwasababu wananchi hawana imani tena na uongozi wa serikali ya kijiji ya sasa.na kama hatuna imani ninaomba mlichukue hilo kwamba wananchi wa kijiji cha Lupalilo hawana imani na serikali yao iliyopo"alisema Zakayo Mahenge


Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Yuda Almasi akizungumza kwenye mkutano huko kwa sharti la kutotaka kurekodiwa sauti yake, amesema tayari alikwisha andika barua ya kukusudia kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti wa kijiji hicho na kilichobaki sasa ni kuipeleka barua hiyo kwenye mamlaka zinazotakiwa


Licha ya wananchi kuzipokea taarifa hizo wameazimia fedha zilizopo kwa mwenyekiti wa kijiji, Afisa mtendaji wa kijiji pamoja na zilizotunzwa na Mwenyekiti wa kamati ya Mipango na fedha wazirudishe 


Afisa Mtendaji wa Kata ya Lupalilo Bw. Sabas Kereth amewataka viongozi wawatumikie wananchi kama inavyotakiwa na si kuichafua serikali kwa kuwa uzembe wa watu wachache usiwafanye wananchi kuiona serikali kuwa haifai, huku diwani wa kata hiyo Mh Imani Mahenge akiwataka viongozi wa kijiji hicho kusoma mapato na matumizi kwa kufuata utaratibu uliopo kisheria.



Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...