Wednesday, February 3, 2021
Wahariri Vyombo Vya Habari Wakoshwa Na Mfumo Wa GePG
Na. Peter Haule na Ramadhani Kissimba, WFM, Arusha
KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla kwa kuweka mfumo imara wa ukusanyaji mapato ya Serikali wa GePG ambao unawawezesha wananchi kulipia huduma mbalimbali za Serikali kupitia mfumo huo.
Akizungumza wakati akifungua semina ya siku mbili kwa Wahariri kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, iliyoanza leo jijini Arusha, amesema kuwa mfumo wa GePG umeimarisha ukusanyaji mapato ya ndani na kuwezesha mwananchi kuwa na uhakika wa malipo mbali mbali yanayofanyika kupitia ( Control Number) ambayo ni salama zaidi katika mchakato wa ukusanyaji mapato.
Amesema, mfumo huo pia unawezesha wananchi kuokoa muda kuanzia anapopata Ankara zake, namna ya ulipaji wake, na upatikanaji wa Stakabadhi yake ikiwa ni pamoja na fedha kufika Serikalini kwa wakati na kuepuka upotevu wa mapato ya Serikali.
''Mfumo huu wa GePG umeimarisha ukusanyaji mapato kwa kuondoa gharama za miamala ya fedha kwa Umma, utaratibu usio rafiki wa ulipaji huduma za Umma pamoja na makusanyo yote kuonekana kwa uwazi na uhakika wa taarifa mbali mbali." Amesema Kwitega.
Aidha, alisema kuwa, mfumo huu umeweza kuongeza mapato mfano Wakala wa misitu Tanzania walikuwa wakikusanya kiasi cha shilingi bilioni 95 kwa mwaka kabla ya mfumo huu wa GePG lakini baada ya kutumia mfumo huo waliweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni.115.
Vile vile, alisema kuwa Shirika la Umeme TANESCO liliweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 38 kwa mwwaka ambazo zilikuwa zikitumika kulipia gharama za wakala kabla ya mfumo huo ambapo baada ya kufunga mfumo huu wameweza kuokoa fedha hizo ambazo zilikuwa gharama za miamala kwa umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi amewataka wahariri kuhakikisha kuwa wanatoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato(GePG) katika kufanya malipo ya huduma mbalimbali za Serikali . Sausi amesema, kabla ya mfumo huo wa GePG kulikuwa na upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kutokana na kutokuwepo kwa uwazi wa ukusanyaji wa mapato pamoja na ukosefu wa taarifa sahihi na kwa wakati.
"Niwaombe wahariri muwaeleze wananchi kuepuka kulipa pesa taslimu kwa kuwa, kwanza hazitafika kwa wakati pili zitapotea na mwananchi ataingia hasara ya kulipa kwa mara nyingine tena, hivyo watumie 'Contorl Number' ili kuepuka upotevu usio wa lazima."amesema John.
Aidha alisema kuwa Mfumo huo umeunganishwa na Taasisi mbalimbali za Serikali za mitaa, Halmashauri, Taasisi na serikali kuu zipatazo 670.
Bw. Sausi alisema mfumo huo ulianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa Taasisi chache ambapo umewezesha kuongezeka kwa mapato kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mchumi Mwandamizi anayesimamia mapato ya Serikali kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Bi. Neema Maregeli alibainisha kuwa mfumo wa GePG umeongeza mapato ya Serikali kutoka wastani wa shilingi bilioni 800 kabla ya Mfumo huu hadi wastani wa trioni 2.4 kwa mwaka.
Alisema kuwa mapato haya yamewezesha Serikali kutekeleza shughuli zake mbalimbali ikiwemo kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Vile vile , alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kupitia wahariri walioshiriki mafunzo hayo kuwaelimisha wananchi kwa ufasaha umuhimu wa kulipa kodi, kudai risiti wanapofanya manunuzi na kwa upande wa wafanya biashara kutoa risiti wanapouza huduma na bidhaa mbalimbali.
MWISHO.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...