Wachunguzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) leo wametembelea kituo cha utafiti katika mji wa Wuhan China, ambacho kimekuwa kikihusishwa na uvumi wa chimbuko la virusi vya corona.
Hatua ya timu hiyo ya WHO kutembelea kituo hicho cha utafiti wa virusi, inaonesha dhamira yao kukusanya data na kutafuta ishara kuhusu ni wapi virusi hivyo vilianzia na vilisambaa vipi.
Kwenye moja ya maabara kubwa ya utafiti katika kituo hicho, kuna sehemu inayohifadhi data za maumbile ya popo, iliyojengwa baada ya mripuko wa homa kali ya kupumua mwaka 2003.
Kutokana na hiyo kumekuwa na uvumi ambao haujathibitishwa kwamba huenda kuna uhusiano wa mripuko huo wa 2003 na wa COVID-19 ulioanza mwishoni mwa mwaka 2019.
China imekuwa ikikanusha vikali uwezekano wowote kama huo na imekuwa ikikuza nadharia kuwa huenda virusi hivyo vilianzia kwingine au labda vilipelekwa nchini humo kupitia bidhaa za kuagizwa, dhana ambayo imepingwa na wanasayansi na mashirika ya kimataifa.
Timu hiyo ya WHO inayowajumuisha wanasayansi kutoka nchi 10, tayari imetembelea hospitali, taasisi za utafiti na pia soko la wanyama