Wednesday, February 17, 2021

Uturuki yamkamata mshukiwa wa IS Syria

 


Walinzi wa mpakani wa Uturuki wamewakamata raia watano wa Urusi, akiwemo mwanamke mmoja anayeshukiwa kuwa mwanachama wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS aliyejaribu kuvuka mpaka kutoka Syria. 


Haijafahamika wazi kama watu wote sita ni washukiwa wa kundi hilo la jihadi. Maafisa wa Uturuki wamesema leo kuwa walinzi hao kwenye kituo cha Hatay katika wilaya ya Narlica, kusini mwa Uturuki waliwakamata watu sita akiwemo raia mmoja wa Libya na watano wa Urusi waliokuwa wanajaribu kuvuka mpaka kinyume cha sheria kuingia Uturuki wakitokea Syria. 


Mmoja wa raia wa Urusi ni mwanamke aliyetambuliwa kama mwanachama wa IS anayetafutwa. Katika tukio tofauti, polisi wa Uturuki wiki hii pia walimkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 26 na watoto wake wawili karibu na mpaka wa Syria. 


Uturuki imeongeza mapambano yake dhidi ya wapiganaji wa IS wanaoendesha mashambulizi kwenye ardhi yake.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...