Thursday, February 18, 2021

Mwanamichezo wa zamani kuongoza kamati ya Olimpiki Japan


Seiko Hashimoto, mwanamke ambaye alishiriki mara saba katika michezo ya Olimpiki amechaguliwa leo kuwa rais wa kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki mjini Tokyo. 

Hashimoto anachukua nafasi ya Yoshiro Moto aliyejiuzulu baada ya kutoa matamshi ya kuwadhalilisha wanawake. Moto mwenye umri wa miaka 83 alijiuzulu baada ya kusema kuwa panapokuwa na wanawake mikutanoni, mikutano hiyo huchukua muda mrefu kwa kuwa wanawake huzungumza sana

Na sasa Hashimoto ametangaza kwamba amechaguliwa katika nafasi hiyo baada ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kama waziri katika baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Yoshihide Suga ambaye amemtaka alete ufanisi katika michezo hiyo ambayo tarehe yake bado haijaamuliwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...