Mbwa mmoja amerithi fedha dola milioni 5 kutoka na mmiliki wake aliyefariki katika jimbo la Tennessee, nchini Marekani.
Taarifa zimearifu kwamba mfanyabiashara Bill Doris, ambaye alifariki katika siku za mwisho za mwaka 2020, alimwachia mbwa wake Lulu wa miaka 8 wa aina ya Border Collie, urithi wa fedha dola milioni 5.
Katika wosia wake, Doris aliomba urithi huo utumike kwa gharama za utunzaji wa mbwa wake Lulu, na malipo ya mwangalizi Martha Burton, atakayepewa kiwango maalum kinachofaa kila mwezi.
Mwangalizi wa Lulu alisema kwamba hajui iwapo ataweza kutumia fedha dola milioni 5 kwa ajili ya mbwa, lakini alitaka kujaribu.
Taarifa zaidi zimebaini mfanyabiashara huyo aliyefariki hakuwahi kufunga ndoa.
Source