Thursday, February 25, 2021

Bobi Wine atakiwa kuelezea jinsi alivyopata gari lake la kifahari


Mamlaka nchini Uganda zinamtaka kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP), Robert Kyagulanyi Sentamu kuweka wazi jinsi alivyopata gari lake jipya la kifahari kufikia Machi 31.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kampala, Mkaguzi Mkuu wa Serikali alitangaza kuwa viongozi wote nchini humo wataanza kutangaza mali zao, vyanzo vyake na madeni waliyonayo kwanzia Machi 1.

Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari, mkurugenzi wa kanuni ya maadili katika ofisi ya mkaguzi wa mkuu wa serikali, Annet Twine, alithibitisha kwamba viongozi watahitajika kutangaza mali zao ikiwa ni pamoja na zawadi na misaada waliopokea katika juhudi za kukabiliana na ufisadi.

Huku hayo yakijiri Waziri wa Maadili na Uadilifu Ethics Fr Simon Lokodo alikariri kujitolea kwa serikali kupambana na ufisadi.

Wiki iliyopita Bw. Kyagulanyi, mgombea wa urais wa zamani, alizindua gari lake jimpya aina ya SUV na Cruiser V8 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja za Uganda, ambalo alidai haliingii risasi .

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...