Saturday, February 13, 2021

Biden anataka kulifunga gereza la Guantanamo Bay


Rais wa Marekani Joe Biden anataka kulifunga gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba linalotumiwa kuwashikilia washukiwa wa ugaidi kabla ya muhula wake kumalizika. 

Msemaji wa Ikulu Jen Psaki amesema hayo wakati alipozungumza na waandishi habari. Gereza hilo la kijeshi lina wafungwa wanaohusishwa na kile kinachoitwa na Marekani "vita dhidi ya ugaidi", akiwemo Khaled Sheikh Mohammed wa Pakistan, ambaye alitangaza kuwa ndiye mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11, mwaka 2001. 

Hadi sasa gereza hilo bado lina wafungwa karibu 40 hadi 26 miongoni mwao wanaochukuliwa kuwa ni hatari iwapo wataachiwa huru

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...