Saturday, January 9, 2021

Uganda yalaumiwa kwa kuwabana wapinzani


Shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu limeilaumu mamlaka nchini Uganda na kusema imekuwa ikitumia janga la Covid-19 kama sababu ya kuuzuia upinzani kushiriki kikamilifu kwenye kampeni za uchaguzi wa rais na bunge unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo. 

Ofisi ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu imesema serikali ya Rais Yoweri Museveni imepunguza idadi ya watu wanaoruhusiwa kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyama vya upinzani kwa kiwango kikubwa na kwamba wagombea wa upinzani na wafuasi wao wanakabiliwa na unyanyasaji, pamoja na kukamatwa kiholela. 

Msemaji wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu Ravina Shamdasani aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba vizuizi hivyo vimewekwa kimakusudi ili kupunguza shughuli za kampeni za uchaguzi kwa upande wa upinzani wakati polisi hawazingatii amri ya vizuizi hivyo katika maeneo ya kampeni za chama tawala.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...