Thursday, January 7, 2021

Twitter, Facebook za Trump Zafutwa





AKAUNTI za Twitter na Facebook za Rais wa Marekani, Donald Trump, zimefutwa kwa muda baada ya kutuma ujumbe kwa wafuasi wake waliovamia bunge la Marekani. Katika ujumbe uliotumwa katika mitandao hiyo kwa waandamanaji, alisema:  'Nawapenda' akiwataka kwenda nyumbani.

 

Pia alizungumzia kuhusu madai ya uongo kuhusu udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi huo. Twitter ilisema kwamba inahitaji kuondolewa kwa jumbe tatu za twitter za rais huyo kwa kukiuka maadili.

 

Kampuni hiyo ilisema kwamba akaunti ya rais huyo itasalia kufungwa kabisa iwapo jumbe hizo za twitter hazitaondolewa. Iliendelea kusema ukiukaji wa sheria za twitter siku zijazo utasababisha kufutiliwa mbali kwa akaunti ya @realDonaldTrump account".

 

Hatua hiyo ina maana kwamba siku za Donald Trump katika mtandao wa twitter zitakuwa hatarini. Rais huyo hajulikani kwa kuheshimu masharti ya muongozo wa twitter kuhusu jamii. Wakati huohuo facebook ilimfuta bwana Trump kwa saa 24 . Youtube pia iliondoa video hiyo.

 

Facebook ilisema: Tuliiondoa kwas ababu tuliamini kwamba inachochea badala ya kupunguza ghasia zilizokuwa zikiendelea. Wafuasi wake walivamia kiti cha serikali ya Marekani na kukabiliana na maafisa wa polisi, kitu kilichosababisha kifo cha mwanamke mmoja.

 

Ghasia hizo zilisitisha mjadala kuhusu ushindi wa rais mteule, Joe Biden. Kabla ya ghasia hizo Rais Trump aliwaambia wafuasi wake mjini Washington kwamba uchaguzi huo uliibwa.

 

Saa chache baadaye ghasia kuzuka ndani na nje ya jumba la Capitol Hill, alionekana katika video akirejelea madai hayo ya uongo. YouTube ilisema kwamba iliiondoa kanda hiyo ya video kwa sababu ilikiuka sera za kusambaza madai ya udanganyifu kuhusu uchaguzi uliopita.

 

Awali Twitter haikuwa imeiondoa video hiyo, na badala yake kuondoa uwezo wake wa kujibiwa, kupendwa na kutolewa maoni. Lakini baadaye iliiondoa na kufuta akaunti ya rais huyo anayeondoka madarakani.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...