Saturday, January 9, 2021

Shule binafsi zalia uhaba wa wanafunzi

 


Wamiliki wa sekondari binafsi wamesema wanakabiliwa na uhaba wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha kwanza baada ya wengi kwenda shule za Serikali.


Suala hilo linadaiwa limetokana wanafunzi wengi waliohitimu elimu ya msingi katika shule hizo wenye daraja A na B kuchaguliwa kujiunga shule za Serikali.


Akizungumza na Mwananchi, mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania (Tamongsco), Leonard Mao alisema mpaka sasa bado shule nyingi hazijajua kiasi cha wanafunzi zitakazowapokeaila mpaka Februari itafahamika zaidi.


Alisema ikilinganishwa na miaka iliyopita, Serikali imechukua wanafunzi wa liopo madaraja ya juu zaidi hasa A, B na C bila kujali kuwa wengi waliopata madaraja ya A na B ni waliotoka shule binafsi.


"Mpaka sasa siyo rahisi kufahamu shule gani haina wanafunzi na ipi ina wanafunzi, matokeo yalipotoka Serikali imewachukua wanafunzi na kuwaacha wenye wastani wa D, hawa walioachwa ndiyo fursa kwetu, wakija kuomba nafasi tunawasajili," alisema Mao.


Mwenyekiti huyo alisema mpaka sasa shule nyingi hazijapata wanafunzi lakini wanaamini wazazi wengi wanasubiri chaguo la pili (second selection) na baada ya hapo wanaamini watapata wanafunzi wa kutosha.


Mao alisema Serikali inapodahili shule binafsi huwa hazishirikishwi, inafanya hivyo ikiwa peke yake.


"Hakuna shule binafsi iliyodahili. Zile zenye shule ya msingi na sekondari waliwachukua wote waliomaliza darasa la saba lakini baadhi unakuta 47 wamechukuliwa na kubaki 50.


"Kuna wazazi ambao watoto wao wamechaguliwa shule za vipaji maalumu na zile nzuri za Serikali wamewapeleka huko kwa maana sisi tunafundisha wanakuwa bora lakini uamuzi wa mwisho mtoto asome wapi ni wa mzazi mwenyewe," alisema Mao.


Hata hivyo, Mao alisisitiza kuwa wazazi wengi ambao watoto wao walifaulu vizuri na kuchaguliwa shule za Serikali wamewapeleka huko kutokana na mkwamo uliotokana na corona. Sisi tumewatengeneza mpaka wamekua bora, sasa Serikali inawachukua kwa kuwa wanafahamu hawatapata taabu kufundisha lugha, tayari wana uelewa mkubwa na ndiyo watakaofanya vizuri au wakadhoofishwa kidato cha nne na sita lakini hawa waliowaacha watakuja kwetu na kidato cha nne watapatikana bora pia," alisema Mao. Mdau wa masuala ya elimu, Benjamin Nkonya alisema hali ni mbaya kwani wanafunzi wanaojiunga shule binafsi wamepungua sana hata ulipaji ada sio mzuri na wamiliki wamekata tamaa, wengine wanauza shulezao.


"Serikali ilipowaondoa wenye vyeti feki, walimu wengi waliofoji na kusababisha shule za Serikali zisifanye vizuri wakaondolewa pia," alisema Nkonya.


Walimu waliobaki, Nkonya alisema wanasimamiwa vizuri na shule ikifanya vibaya walimu wakuu wanaondolewa hivyo kukabili udhaifu uliokuwapo ambao ulizifanya shule binafsi zionekane ni bora zaidi kuliko za umma.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...