Friday, January 8, 2021

Rais wa Zimbambwe Aisuta Marekani Baada ya Bunge Kuvamiwa



Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amezungumzia vurugu zilizotokea Marekani baada ya wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia jengo la bunge Capitol Hill.

Bwana Trump alichochea wafuasi wake kuandamana hadi bungeni ili kuvuruga kikao cha kumuidhinisha Rais mteule kilichokuwa kinaendelea.


Rais Mnangagwa aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa Marekani haina "haki ya kimaadili kuadhibu nchi zingine kwa misingi ya demokrasia".


Alisema kuwa Marekani imeiwekea Zimbabwe "vikwazo vikali" vya kiuchumia.


"Ningependa tena kumpongeza Rais mteule Joe Biden, kwa kuthibitishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani.


"Zimbabwe iko na imekuwa tayari ushirikiano wake kama marafiki na washirika wa Marekani kwa manufaa ya nchi zote mbili," Bwana Mnangagwa amesema.


Marekani na Umoja wa Ulaya zote zimeendeleza vikwazo vyao dhidi ya Zimbambwe kwa madai ya ukosefu wa demokrasia endelevu na mabadiliko ya haki za binadamu pamoja na kubanwa kwa vyombo vya habari.


Wanalenga watu binafsi na makampuni.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...