Wednesday, January 27, 2021

Rais Putin: Urefushwaji wa mkataba wa New START ni njia sawa

 


Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema makubaliano na Marekani kurefusha muda wa mkataba wa kudhibiti matumizi ya silaha za kimkakati za nyuklia kwa miaka mitano, ni hatua nzuri katika kupunguza mivutano ulimwenguni.

Akizungumza kwa njia ya video kwenye Jukwaa la Kiuchumi Duniani mjini Davos, Putin amesifu hatua hiyo iliyofikiwa baada ya mazungumzo yake na rais wa Marekani Joe Biden kwa njia ya simu.

Lakini ameonya kuwa hali zisizotabirika na zisizodhibitika zinaweza kujitokeza ulimwenguni ikiwa hawatochukua hatua yoyote.

Mapema leo, mabunge yote mawili ya Urusi yaliidhinisha urefushwaji wa mkataba huo ambao muda wake ulitarajiwa kumalizika Februari 5.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Matvienko amesema baada ya kura, kwamba urefushaji wa mkataba huo utaanza kutekelezwa wakati pande zote mbili zitabadilishana nakala taratibu zote zikimalizika.Urefushwaji wa mkataba huo hauhitaji kuidhinishwa na mabunge ya Marekani.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...