Watoto pacha, Dorcas na Dorine waliozaliwa wameungana katika hospitali teule ya wilaya ya Iringa Tosamaganga wamefariki dunia.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Ismail Banoba amethibitisha na kubainisha kuwa walipata shida ya upumuaji kwa kuwa wana moyo mmoja.
