Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga amekemea vitendo vya udhalilishaji kwa Watu wenye Ulemavu ikiwemo kuwatumia ili kujinufaisha
Naibu Waziri ameeleza kuwa, kumekuwa na vitendo vya udhalilishaji kwa Watu Wenye Ulemavu ambavyo vimekuwa vikiendelea katika Jamii na vitendo hivyo vinapelekea ukiukwaji wa haki
Amebainisha kuwa, wapo baadhi ya watu ambao ni kama Mawakala na wanawatoa Watu Wenye Ulemavu katika Mikoa mbalimbali na kuwaleta Dar es Salaam kwa lengo la kuwafanya ombaomba mitaani huku kila siku anachukua fedha hizo kwa maslahi binafsi
Akiweka msisitizo kuhusu udhalilishaji huo, Ummy aliwachapa viboko baadhi ya vijana ambao wamekuwa walishiriki kudhalilisha Watu Wenye Ulemavu kwa kuwazungusha kuombaomba mitaani na kisha kuchukua fedha walizokusanya
Aidha, Waziri Ummy amewataka Wananchi kutowaonea aibu wahusika wanaofanya vitendo hivyo badala yake wawe huru kutoa taarifa katika Vyombo vya Sheria ili wachukuliwe hatua