Mwanamke mmoja amejinyonga kwa kutumia kanga kwenye mti wa mwembe katika kijiji cha Itununu wilayani hapa, kwa madai ya wivu wa mapenzi, huku akiwa na mimba ya miezi tisa.
Hilo ni tukio la pili la watu kujinyonga katika mazingira ya utata.
Januari 5, saa 11 jioni mwaka huu, Buroi Motera (38) mkazi wa kijiji cha Masangura alijinyonga kwa kamba pembeni mwa nyumba yake, akidaiwa kukwepa hukumu ya kesi ya jinai namba 115/2020 ya wizi wa mifugo iliyokuwa itolewe Januari 11, mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alithibitisha Mkami Nyamhanga (21) kujinyonga Januari 17 kwenye mti wa mwembe uliopo shambani.