Saturday, January 9, 2021

"Milioni 35 kwangu ni kitu cha kawaida" - Pili

 

Ni mbwem
bwe za producer na mchekeshaji Pili Kitimtim ambaye amesema hategemei pesa za mwanaume ili kuendesha maisha yake, kama ni gari yenye thamani ya Milioni 35 hata yeye anaweza kununua na ni kitu cha kawaida kwake.


Kupitia EATV & EA Radio Digital, Pili Kitimtim amesema hamchuni mwanaume wake pesa wala halipiwi kodi na matumizi mengine ila anachotegemea kutoka kwa mpenzi wake huyo ni furaha mawazo na kushauriwa.


"Mimi na mpenzi wangu tunashindana kiuchumi,  kwenye gari zangu zote 3 hajatia hata elfu 5, hanilipii kodi na mimi simlipii kwa sababu wote ni vijana tunatafuta na hatuchunani, kwenye mahusiano yetu gari ni kitu cha kawaida kama ni milioni 35 kwangu ni kitu cha kawaida nanunua" amesema Pili Kitimtim 

VIDEO:



Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...