Thursday, January 7, 2021

Jeshi na polisi wavamia bunge Ghana




Vikosi vya usalama nchini Ghana vimevamia bunge siku ya Jumatano kufuatia ghasia zilizoibuka kati ya chama tawala na chama kikuu cha upinzani.
Vurugu hiyo ilianza kutokana na kuchaguliwa kwa spika mpya wa bunge kuapishwa.

Jeshi na polisi walivamia kwa kipindi cha dakika 10 kabla ya kutoka nje kila mmoja akiwa amemshikilia mbunge mmoja.

Chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC) kilifungua kesi katika mahakama kuu kupinga matokeo cha uchaguzi yaliyopelekea kumpa ushindi rais Nana Akufo Addo katika uchaguzi wa mwezi Desemba.

Chama hicho kinataka majaji kutoa ruhusa ya uchaguzi kurudiwa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...