Tuesday, December 1, 2020

Wazazi wa watoto shule ya St Jude waeleza sababu ya kuandamana


Wazazi zaidi ya 1,000 wa wanafunzi wanaopatiwa ufadhili wa masomo katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya St. Jude iliyopo Arumeru mkoani Arusha, wameandamana  hadi ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kulalamikia hatua ya watoto wao kusitishiwa masomo kinyume na utaratibu.


Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba mosi, 2020 wazazi hao waliituhumu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  mkoani hapa kufungia akaunti za mfadhili wao, jambo lililosababisha shule kushindwa kujiendesha ikiwemo kuwahudumia watoto.


Salma Mohamed na Latifa Jafari, wakazi wa jijini hapa wamesema katika kipindi cha wiki mbili watoto wao wamesimamishwa masomo kwa madai shule inadaiwa, hivyo kuiomba Serikali kuwaruhusu kuendelea na masomo.


Wazazi hao pia wanaituhumu  TRA kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti ya shule na kusababisha kushindwa kujiendesha.


Akizungumzia tuhuma hizo, meneja wa TRA mkoa wa Arusha, John Mwigura alikiri kuidai kodi ya muda mrefu shule hiyo,  lakini St Jude ilikataa deni hilo kwa madai haifanyi biashara, hivyo haiwezi kulipa kodi na kukimbilia ngazi mbalimbali ikiwemo  Mahakama ya Rufaa kupinga tuzo la kodi akibainisha kuwa mahakamani  TRA ilishinda kesi hiyo na St Jude iliamuliwa kulipa kodi hiyo.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...