Thursday, December 24, 2020

Uchaguzi wa Uganda 2021: Pendekezo la viongozi wa Kidini kutaka uchaguzi kuahirishwa lapingwa

Serikali ya Uganda kupitia kwa msemaji wake Ofwono Opondo imepinga ombi la Baraza la Muungano wa Madhehebu ya Wakristo nchini Uganda (UJCC) kutaka uchaguzi mkuu ujao wa kuahirishwa kwa madai kwamba viongozi hawatilii maanani kanuni za kudhibiti virusi vya corona.

Bw. Opondo badala yake amesema jambo muhimu ni Tume ya Uchaguzi kupiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya kufanya mikutano ya watu wasiozidi 200 kama inavyotakiwa na watalaam wa afya.

Siku ya Alhamisi mwenyekiti wa baraza hilo Askofu Mkuu wa Kampala Dk. Cyprian Lwanga Kizito kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, alisema kwamba viongozi wa siasa nchini hawazingatii kanuni zilizotolewa za kudhibiti virusi vya corona, na kuleta hofu kubwa baada ya kumalizika kwa zoezi la uchaguzi kutakuwa na vifo vingi zaidi.

''Siku chache zilizopita muungano wa madhehebu ya Kikristo ambayo mimi ni mwenyekiti, tulitafakari hali ilivyo kwa sasa nchini na kuafikiana kwa pamoja kwamba waahirishe uchaguzi wa urais ili kuruhusu kudhibiti virusi vya corona na kuteremsha moto wa wanasiasa, kujenga mazingira mazuri ya siasa kuleta uchaguzi huru na wa amani . Haya ni mapendekezpo hivyo tunatoa wito kwa bunge kulijadili hili.'',alisema Askofu Mkuu Kizito.

Baraza hilo pia linataka katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho ili kumuruhusu rais Museveni kuendelea kutawala katika kipindi hicho.

Pia amesema kuwa vikosi vya vya ulinzi vikiendelea kufanya vitendo vya kikatili kwa wananchi na kuleta maafa makubwa, ndiyo sababau wanaomba serikali kuhayirisha zoezi hilo kama anavyoelezea.

Kwa upande wake Akol Amazima ni mchambuzi wa siasa ametofautiana na viongozi wa dini akisema :Itabidi kwanza katiba ibadilishwe kwasababu katiba inasema kila baada ya miaka mitano. Kwa hivyo naona tunaelekea mwisho wa uchaguzi na sasa hivi itakuwa vigumu kusema kwamba uchaguzi uahirishwe''

Bw. aliendelea kusema kuwa Uganda sio nchi ya kwanza kufanya uchaguzi wakati kuna janga la corona, Malawi walifanya uchaguzi, Burundi walifanya uchaguzi, Ghana, Burkina Faso, Ivory Coast wote wamefanya uchaguzi. Janga hili yaani mwisho wake utakuwa lini.

Pia ameongeza kuwa suala la kusema joto la kisiasa limepanda halina msingi wowote ''Kwa kawaida hapa nchini Uganda tunapokuwa na uchaguzi joto la kisiasa linapanda, Tanzania wamekuwa na uchaguzi na joto la kisiasa lilikuwa juu sana. Hivyo ndivyo ilivyo hali ya demokrasia barani Afrika

Tangu kuanza kampeni za uchaguzi tarehe 9 mwezi wa kumi na moja wagombea wa kiti cha rais wengi wao wameshindwa kufata kanuni za watalaam wa afya na kusabaisha jeshi la polisi kutumia vitoa machozi na hata risasi kuwatawanya watu.

Uganda inafanya kitu kinachoitwa "Uchaguzi wa Kisayansi". Unaitwa hivyo kwa sababu Tume ya Uchaguzi iliamua kwamba kwa sababu ya ugonjwa wa Corona (Covid 19), taratibu za mikusanyiko kama ilivyozoeleka wakati wa kampeni hazitakuwepo tena.

Hii maana yake ni kwamba washindani sasa wanafanya zaidi kampeni kupitia vyombo vya habari kuliko mikutano ya hadhara kama ilivyozoeleka.

Jambo hili lina faida zaidi kwa chama tawala kuliko wapinzani.

Chama tawala kinatumia vyombo vya habari vya umma kujipigia kampeni wakati wapinzani hawana fursa hiyo.

Mikutano ya hadhara ni muhimu kwa vyama vya upinzani kuliko chama tawala kwa sababu zaidi ya moja.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...