Tuesday, December 15, 2020

Rasmi Wajumbe waidhinisha ushindi wa urais wa Joe Biden



Joe Biden amesema kuwa "utashi wa watu umeshinda " baada ya ushindi wake wa uchaguzi kuthibitishwa na wajumbe wa uchaguzi wa Marekani – US electoral college.

Katika hotuba aliyoitoa baada ya kutangazwa kwa ushindi huo , alisema kuwa demokrasia ya Marekani "imesukumwa na kujaribiwa " na "imedhihirisha kuwa ni jasiri, ya kweli na thabiti ".

Bw Biden pia amezungumzia kuhusu hatua ya Trump ya kujaribu kupinga matokeo ya uchaguzi.

Kuthibitishwa kwa ushindi huo ni mojawapo ya hatua alizohitaji Bw. Biden ili kumuwezesha kuchukua mamlaka ya urais.

Chini ya mfumo wa Marekani, wapiga kura hupiga kura zao kwa "wachaguzi ", ambao hatimae huwachagua wagombea wao wiki kadhaa baada ya uchaguzi.

Mdemocrat Joe Biden alishinda katika uchaguzi wa Novemba kwa kura 306 za wajumbe dhidi ya Mrepuublican Donald Trump ambaye alipata kura za wajumbe 232.Wajumbe walimuidhinisha Biden kama rais mteule wa Marekani

Wajumbe walimuidhinisha Biden kama rais mteule wa Marekani
Rais Trump bado hajatoa kauli yoyote. Muda mupi baada ya matokeo kuthibitishwa, alitangaza kwenye ukurasa wa Twitter kuondoka madrakani kwa Mwanasheria Mkuu William Barr, ambaye alisema kuwa hapakuwa na wizi ushahidi wa wizi wa kura katika uchaguzi, licha ya madai ya rais.

Akizungumza katika jimbo la Delaware, Bw Biden alisifu wale aliowaita "wanaume na wanawake wa kawaida " ambao walikataa kunyanyaswa, akizungumzia juhudi za rais za kuhoji na kubadilisha matokeo ya uchaguzi , akihusisha mashitaka ya kisheria ambayo yamekuwa yakikataliwa na mahakama kote nchini Marekani.

"Moto wa demokrasia uliwaka zamani katika nchi hii ," alisema . "Na tunafahamu kwamba hakuna lolote hata janga la ugonjwa au ukiukaji wa mamlaka unaweza kuzima mioto hiyo ."

Bw Biden alisema kuwa ni muda wa "kugeuza ukurasa, kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika kipindi chote cha historia -kuungana na kupona".

Nini kilichotokea katika taasisi ya kura za wajumbe?
Kwa kawaida wajumbe wanaochagua huwa hawafuatiliwi sana lakini mwaka huu, kutokana na juhudi za Bw Trump kura ya jimbo hadi jimbo kilikuwa inafuatiliwa.

Jimbo la Califonia ambalo ni ngome ya Democratic lilikuwa la mwisho kupiga kura Jumatatu na kumuwezesha Bw Biden kupata kura 270 -zinazohitajika kushinda urais.

Ulinzi mkali uliimarishwa katika baadhi ya majimbo, ikiwa ni pamoja na Michigan na Georgia,kabla ya upigaji kura kufanyika katika miji mikuu ya majimbo na mji mkuu wa Marekani Washington DC.

Katika jimbo la Michigan -jimbo muhimu ambalo halitabiliki inapokuja katika matokeo ya uchaguzi ambako Bw Biden alishinda-sajili katika mji mkuu Lansing zilifungwa kutikana na vitisho "vya kuaminika " vya ghasia.

Kura katika jengo la capitol iliendelea kupijgwa kwa amani ingawa kikundi cha Warepublican kilijaribu kuingia katika jengo hilo kuendesha kura yao lakini walifukuzwa.Rais wa Marekani hachaguliwi mara moja na wapigakura,bali kile kinachoitwa electoral college

Rais wa Marekani hachaguliwi mara moja na wapigakura,bali kile kinachoitwa electoral college
Katika hotuba yake Bw Biden alielezea unyanyasaji wa maafisa kufuatia uchaguzi kama kitendo "kisicho haki " alisema : "Ni matumaini yangu kuwa hatutashuhudia mtu mwingine akipitia aina hii ya vitisho na unyanyasaji tuliouona katikauchaguzi huu."

Nini kitakachofuata?
Matokeo ya mchakato wa upigaji kura yatatumwa Washington DC na kuhesabiwa katika kikao cha pamoja cha Congress tarehe 6 Januari kinachoongozwa na Makamu wa rais Mike Pence.

Hiyo itatoa fursa kwa Joe Biden kuapishwa kama rais wa Marekani tarehe 20 Januari.

Mwezi uliopita , Rais Trump alisema kuwa ataondoka ofisini kama Bw Biden ataidhinishwa kama mshindi na wajumbe wa uchaguzi . Hatahivyo , amekuwa akiendelea kutoa madai ambayo hayana ushahidi ya wizi wa kura na kuna ishara chache kwamba atakubali kushindwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...