Sunday, December 27, 2020

Mwakamo awapa somo wafanyabiashara Mlandizi


 

Na Omary Mngindo, Mlandizi.

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo amewataka wafanyabiashara wa mchele kuanza maandali ya kutafuta eneo, kupisha mradi wa barabara unaotaraji kupita.

Aidha amewashauri kipindi hiki kuchangamkia ardhi katika maeneo yanayopimwa pembezoni mwa mji, ili ujenzi wa barabara unaotokea Makofia Bagamoyo mpaka Mlandizi utakapokuwa tayari wawe tayari wana eneo mbadala.

"Rais wetu Dkt. John Magufuli akiwa hapa alisema kwamba kuna ujenzi mkubwa wa barabara itokayo Bagamoyo, Mlandizi mpaka Mzenga Kisarawe, ukichanganya na inayotokea Dar es Salsaam kuelekea Chalinze ni wazi kwamba hapa hatutosalimika," alisema Mwakamo.

Alisema kwamba hivi sasa kuna upimaji mkubwa wa ardhi maeneo ya Kwala eka elfu nne, Mkino, Ngeta na Kikongo ambapo alisema ni wakati wa kuchangamkia fursa hiyo, huku mwanamama anayeuza mchele akisema nje ya eneo hilo watakosa wateja.

Kuhusu hilo Mwakamo alisema kwamba wateja wanafuata huduma ilipo, huku akitolea mfano wa soko la Loliondo Kibaha Mji na maeneo mbalimbali, ambapo aliwaambia mchele wanaouza unanunuliwa na kusafirishwa nchi za nje.

"Japokuwa wenyewe mnajiona hamna nguvu, lakini niwaambie kwambana nguvu kubwa mnaolingana na wafanyabiashara wengine, huu mchele mnaouza kulo mojamoha mkimpata mtaalamu akiugeuza fedha mna mtaji mkubwa," alimalizia Mwakamo.

Akiongelea ujenzi wa barabara hiyo alisema kwamba eneo la Mlandizi njiapanda ya Bagamoyo Mzenga na Dar es Salaam Chalinze kutakuwa na mzunguko (round about) ambayo itachukua mzunguko mkubwa utaosababisha eneo hilo kutokuwepo, hivyo wachangamkie maeneo yanayopimwa.

Aidha amewaambia kuwa umoja huo ni mtaji mkubwa, huku akiwataka waunde uongozi utaowezesha kuunda umoja utaowezesha kufanikisha mambo mbalimbali ikiwemo kupata ardhi yenye hati itayowawesesha kuwa na uwezo wa kukopa kisha kufanya mambo makubwa.

Kwa upande wao wafanyabiashara hao Ally Ramadhani alizungumzia kupatiwa mikopo, ambapo Mwakamo alisema cha msingi ni kukaa pamoja kutengeneza mpango itaowafanikishia malengo makubwa ambayo wamejiwekea.

Nae mmoja wa wafanyabiashara hao amemwambia Mbunge huyo kwamba ushauri huo wameupokea na kwamba watakwenda kuufanyiakazi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...