Sunday, December 27, 2020

Mkenge afanikisha wanafunzi 184 kupatiwa vifaa


 

Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge kupitia taasisi ya Lady Fatemah Trust (UK) imewapatia wanagunzi 184 madaftari na mikebe ya kuwekea kalamu, peni na lura.

Msaada huo umetokana na Mkenge kuwasiliana na uongozi wa taasisi hiyo inayosaidia wanafunzi wa kike, umelenga kuwasaidia wazazi na walezi wa watoto hao ambapo vikitumika vizuri vinaweza kuwasaidia kipindi cha mwaka mzima.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa madaftari hayo na mikebe yenye kalamu, peni pensel na lura, Mkenge aliwashukuru wadau hao, huku akiwataka kuendeleza ushirikiano zaidi katika uboreshaji wa vyumba vya madarasa shuleni hapo ambavyo vinahitaji ukarabati.

"Nawashukuru kwa msaada huu mkubwa mliotupatia, kwaniaba ya wazazi, walezi na wana-Bagamoyo tunawashukuru, pia niwaombe tuendelee kushirikiana katika uboreshaji wa vyumba vyetu vya madarasa kama mlivyoviona," alisema Mkenge

Kwa upande wake diwani Aspsa Kilingo akizungumza kwa niaba ya wazazi alishukuru msaada huo, huku akiwaomba wazazi kuvitunza ili viwasaidie wanafunzi kwa kipindi cha mwaka, kwani vinaweza kuwafikisha endapo watavitunza.

"Huu msaada ni mkubwa, kama vitatunzwa vizuri vitawasaidia walengwa kuendelea na masomo yao kwa mwaka mzima, hivyo kuwaondolea wazazi gharama za kununua kama ilivyokawaida," alisema Kilingo.

Mwalimu Mkuu Ally Hiza alisema kuwa pamoja na msaada huo mkubwa kwa wanafunzi hao, lakini shule inakabiliwa na changamo ya chumba cha kuwekea kompyuta ikiwemo uchakavu wa paa kutokana na kuwepo jirani na Bahari.

Akizungumzia taasisi hiyo na kazi inazozifanya, Talib Shariff alisema kwamba wamelenga zaidi kusaidia wanafunzi wa kike, lengo kuona wanafanikisha malengo yao ya kielimu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...