Friday, December 4, 2020

Kuwait inasema mjadala wenye tija kusuluhisha mzozo na Qatar


Kuwait imesema kumekuwepo mjadala wenye tija wa kusuluhisha mzozo wa muda mrefu wa Qatar na mataifa manne ya Kiarabu. 


Televisheni ya taifa ya Kuwait imetangaza taarifa hiyo hii leo iliyotolewa na waziri wa mambo ya kigeni, Sheikh Ahmed Nasser Al Mohammad Al Sabah iliyosema kiongozi wa taifa hilo amekuwa na mazungumzo na rais Donald Trump wa Marekani.


Sheikh Ahmed amesema wote wana matumaini kwamba hatimaye kupatikana matokeo ya mwisho ya amani kati ya mataifa yote ya baraza la ushirikiano wa mataifa ya Ghuba. Aidha amemshukuru mkwe wa Trump, Jared Kushner ambaye pia ni mshauri mwandamizi wa Trump, aliyezuru ukanda huo. 


Bahrain, Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu walikata mahusiano ya kidiplomasia na Qatar Juni 2017, wakidai kwamba Qatar inayaunga mkono makundi ya itikadi kali kwenye ukanda huo, madai ambayo Doha inayakataa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...