Tuesday, December 15, 2020

Jafo afungua miradi yenye thamani Zaidi ya bilioni 6 Mkaoni Mtwara


Na Faruku Ngonyani , Mtwara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jaffo hii leo amefungua miradi ya maendeleo yenye thamani Zaidi ya bilioni sita(6)iliyopo Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara.

Moja ya miradi hiyo iliyofunguliwa na Mhe Jaffo ikiwa ni pamoja na barabara ya COTC iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 0.9  iliyoghalimu Zaidi ya Bilioni moja.

Lakini pia Waziri Jaffo amefungua soko la kisasa la Chuno lililojengwa kata ya Chuno Manispaa Mtwara Mkindani lenye thamani ya Zaidi ya bilioni tano.

Selemani jafo amechukua fursa hiyo kwa kutoa wito kwa wananchi wa Manispaa Mtwara Mikindani kuitunza miradi hiyo ili iendelee kuleta taswira ya mji wa Mtwara.

Awali Waziri Jaafu amesema kuwa kwa sasa amepewa dhamana na Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania wa kusimamia barabara zenye urefu wa km laki moja na nane pointi tisa,na katika barabara hizo baraba kadhaa zinapatikana katika miji, Halmashauri Majiji na Manispaa .

Jafu ameeleza kuwa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania alitenga zaidi trion 2.1 lengo ni kutengenezwa kwa barabara hizo ili ziweze kukamilika kwa kiwango cha lami   

Jaffu ameipongeza Manispaa Mtwara Mikindani kwa kusimamia na kuitekeleza miradi hiyo kwa ubora na thamani ya pesa iliyotumika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gellasius Byakanwa amesema kuwa kwa sasa Mkoa utaendelea kusimamia miradi yote ya maendeleo ili iendelee kutunza na kuleta manufaa kwa wananchi na Mkoa kwa ujumla.

Aidha Byaknwa amechukua fursa hiyo kwa kumshukuru Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kwa kuitazama Mtwara na kuleta miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Lakini pia ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa ya miradi hiyo kwa kuongeza uchumi wao lakini pia kuufanya Mji wa Mtwara kuchangamka Zaidi na hatamae kuwa Jijiji.

"Mh.Waziri yamesemwa mengi kuhusiana na miradi uliyoizindua ,mimi nikuhakikishie kwamba miradi hii itatekelezwa  kwa thamani ya pesa iliyotolewa lakini pia kwenye miradi ya kimakakati nitumie fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuingalia Mtwara kwa jicho la pekee, Mtwara ya mwaka 2005 ni tofauti na Mtwara ya mwaka 2020"Byakanwa.

Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani ni miongoni mwa Miji ya kimakati Tanzania (TSCP) unaotekelezwa kwa mkopo wa fedha toka Benki ya Dunia chini ya usimaminzi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...