Friday, December 4, 2020

Guterres azikosoa nchi zilizopuuza mwongozo wa WHO wa corona


 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hapo jana bila ya kuzitaja kwa majina alizilaumu nchi ambazo zilipuuza ushauri wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu janga la virusi vya corona. 

Guterres aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao maalumu kuhusu ugonjwa huo wa COVID-19, kilichojumuisha mataifa wanachama 193 wa umoja huo.

Katibu mkuu huyo alisema mara tu baada ya kuzuka janga hilo, shirika la WHO lilitoa mwongozo wa kisayansi ambao mataifa mengi yalikataa kuufwata.

Rais Donald Trump wa Marekani mapema mwaka huu alizuia ufadhili kwa shirika hilo la WHO na kutishia kuitoa nchi yake, huku akilishutumu shirika hilo kuwa ni kibaraka cha China. Madai ambayo WHO inayakana.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amaeahidi kubatilisha uamuzi huo wa Trump dhidi ya WHO.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...