Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amezitaka pande hasimu katika uchaguzi wa Marekani kuonesha ustahimilivu hadi matokeo kamili ya uchaguzi wao yapatikane, na kuongeza kuwa si wajibu kwao kuzidisha mvutano.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari cha Ujerumani, alisema Marekani ni zaidi ya onyesho la mtu mmoja, na kwamba yeyote anaemwaga mafuta kwenye moto kama inavyoonekana kipindi hiki, anafanya vitendo visivyo vya uwajibikaji.
Katika taarifa yake hiyo ya kwanza kabisa kuhusu uchaguzi wa Marekani amenukuliwa akisema "Sasa ni muda wa kuwa watulivu kabisa, mpaka matokeo yatakapo tolewa.
Trump ameanzisha madai kadhaa katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi kwa lengo la kupunguza kasu ya mpinzani wake Joe Biden, hatua ambayo imezusha hali ya wasiwasi katika taifa hilo kubwa kabisa duniani.