Rais wa Marekani Donald Trump amemsamehe Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa zamani wa masuala ya usalama wa kitaifa, na ambaye alikiri kusema uongo mbele ya shirika la kijasusi la Marekani FBI.
Flynn, ambaye alifutwa kazi mapema katika utawala wa Trump, alikiri kusema uwongo kuhusu kufanya mazungumzo na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergey Kislyak.
Baadae Flynn alibadili msimamo akisema matamshi yake yanapaswa kutupiliwa mbali kwasababu ni mwathiriwa wa madai ya utovu wa nidhamu.
Flynn alikuwa mmoja wa wasaidizi wa Trump kukiri makosa au kutiwa hatiani katika uchunguzi wa Robert Mueller uliohusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa 2016.
Rafiki wa muda mrefu wa Trump na mshauri Roger Stone alihukumiwa madhabu ya miaka mitatu na miezi minne gerezani kwa kuzuia haki, na kusema uwongo kwa wabunge waliokuwa wakichunguza madai hayo.