Wednesday, November 4, 2020

Tani 3,361 za korosho ghafi zanunuliwa RUNALI


Na Ahmad Mmow, Ruangwa. 

Tani 3,361 na kilo 554 ziliuzwa jana na chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi. 

 Katika mnada huo wa nne kwa chama hicho na wanane kwa mkoa wa Lindi kwa msimu wa 2020/2021 bei ya juu ilikuwa shilingi 2,450 na bei ya chini ni shilingi 2,313 kwa korosho daraja la kwanza na shilingi 2,000 kwa korosho daraja la pili ambazo ni tani 30,077.

Katika mnada huo uliofanyika Ruangwa katika viwanja vyo ofisi ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) korosho ghafi hizo zilizopo katika maghala sita yaliyopo katika wilaya za Liwale, Ruangwa na Nachingwea kampuni 21 ziliomba kununua. 

Huku ikishuhudiwa bei 140 tofauti.

 Katika ghala la Lipande lenye tani 1,117 na kilo 112 zimenunuliwa na kampuni za MGM, UDHAYA na Alfa crast. Mbali na kampuni hizo, lakini pia kampuni tatu  zilinunua kwa njia ya mtandao kupitia soko la bidhaa Tanzania(TMX). 

Ambapo bei ya juu ilikuwa shilingi 2,450 na bei ya chini shilingi 2,407.Kwenye ghala la Pachani ambalo korosho zake zilinunuliwa na kampuni za Hajar, Amea na Udhaya lina korosho zenye uzito wa tani  497.46 bei ya juu ni shilingi 2,450 na bei ya chini ni shilingi 2,415.

ion Agro, Amea, Paramount na Alfa crast ni kampuni zilizofanikiwa kununua korosho zenye uzito wa tani 389 na 200 zilizopo katika ghala kuu la Kilimani road ( Zuma Cargo). Ambapo bei ya juu ni shilingi 2,435 na bei ya chini shilingi 2,424.

 Aidha katika ghala la Lindi farmers lenye tani 489 na kilo 295 kampuni za Amea, Hajar, NGM na Export  zimenunua korosho hizo kwa bei ya juu ya shilingi 2,429 na bei ya chini shilingi 2,415.

 Mbali na maghala hayo matano yaliyopo katika wilaya za Nachingwea na Ruangwa. Lakini pia korosho ghafi za daraja la kwanza na pili zimenunuliwa katika ghala la Umoja lililopo wilayani Liwale bei ya juu ilikuwa shilingi 2,350 na 2,315 kwa tani 878 na kilo 901

 Lakini pia ghala hilo lina korosho ghafi zenye uzito wa tani 30,077 ambazo zimenunuliwa kwa shilingi 2,000 kwa kila kilo moja. Kampuni zilizo nunua korosho hizo ni MGM, Paramount, Alfa Crast, Golden na SIBATANZA.

[08:36, 11/4/2020] Kayanda: ¥ Akizungumza baada ya wakulima kuridhia kuuza kwa bei hizo, mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika wa mkoa wa Lindi, Edmund Masawe alisema takribani tani tatu zisizo na ubora (chafu) zimekamatwa katika wilaya za Lindi vijijini na Nachingwea zikiwa zimechanganywa na korosho safi.

Kufuatia hali hiyo, Masawe alitoa wito kwa wakulima na wananchi kwa jumla wasaidie kuwafichua watu wanaoingiza korosho chafu mkoani humo. 

 Alisema korosho chafu zinasababisha ugumu wa kuuza. Kwahiyo hawanabudi kushirikiana na mamlaka ili kulinda uboro utakaovutia wanunuzi watakaosababisha ziweze kununuliwa kwa bei nzuri. 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...