Thursday, November 5, 2020

Mchakato wa mazungumzo kati ya Jumuiya ya Ulaya na Uingereza unatarajiwa kuendelea

Msimamizi mkuu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wa Mchakato wa Brexit Michel Barnier, alisema kuwa bado kuna tofauti kubwa zinazoendelea katika mazungumzo ya makubaliano yatakayounda uhusiano wa kibiashara na Uingereza.

Barnier alitoa maelezo kupitia mtandao wa kijamii kuhusu mchakato unaoendelea kati ya Uingereza na EU.

Katika maelezo yake kuhusu aliyotoa kuhusu mchakato huo unaohusisha wanachama 27 kutoka baraza la bunge la Ulaya, Barnier alisema,

''Licha ya EU kujaribu kutafuta suluhisho, bado kuna ushindani na utofauti mkubwa katika usimamizi wa maeneo ya uvuvi na mahusiano yao kwa ujumla.''

Akibainisha makubaliano hayo kuwa na umuhimu mkubwa wa kiuchumi kwa ushirikiano wa Uingereza na EU, Barnier alisema,

''EU ipo tayari kwa matukio ya aina zote.''

Wawakilishi wa EU na wa Uingereza wanatarajiwa kuendeleza mazungumzo yao wiki ijayo mjini London.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...