Saturday, October 24, 2020

Vijiji vitatau Makete vyakabidhiwa hati miliki ya ardhi za kimila


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kutokana na juhudi za serikali ya mkoa wa Njombe kuhakikisha wananchi wanapata uhalali katika kumiliki ardhi.Hati miliki za kimila 54 zimetolewa na kukabidhiwa kwa wakazi wa kijiji cha Usungilo wilayani Makete huku hati 131 zikiwa zimetolewa mpaka sasa kwa vijiji vitatu vya Makangarawe,Usungilo na Ihela.

Aidha kufuatia Kuanzishwa kwa ofisi ya kamishna wa ardhi kila mkoa ikiwemo mkoa wa Njombe,Mkuu wa wilaya Veronika Kessy aliyekuwa mgeni wa heshima wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo ametumia fursa Hiyo kuwataka maafisa ardhi Kuhakikisha kila ardhi katika wilaya ya Makete inakuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi.

"Kwa fursa amabyo tumepata sasa kwamba tuna kiongozi wa ardhi ngazi ya mkoa tunaomba muhakikishe kwamba vijiji vyetu vinafanya mpango wa ardhi,lakini pia yapo maeneo ambayo miji yetu inakuwa ambayo inatakiwa haraka sana muende mkafanye mpango mji"alisema Veronika Kessy

Shirika la SUMASESU linalotekeleza shughuli za maendeleo katika wilaya ya makete kwa kushirikiana  na halmashauri ya wilaya hiyo limekabidhi jumla ya hati za kimila za umiliki wa ardhi 131 katika vijiji vya usungilo , Makangalawe na Ihela ikiwa ni muendelezo wa kutatua na kudhibiti migogoro ya ardhi.

Awali akitoa taarifa kwa mgeni Rasmi Mkurugenzi wa shirika la SUMASESU Egnatio Mtawa amesema Jumla ya Hati 131 zimetolewa kwa wananchi wa Vijiji hivyo vitatu.

"Kwa kuanza zoezi hili limefanyika katika vijiji vitatu ambavyo ni Usungilo,Makangalawe na Ihela.Jumla ya hati 131 zimetengenezwa na ofisi ya ardhi Makete ikiwa Usungilo hati 54,Makangalawe 34 na Ihela 43 ili kuhakikisha ardhi ndani ya wilaya ya Makete inamilikiwa na wananchi wenyewe" alisema Egnatio Mtawa 

Baadhi ya wananchi Akiwemo Elvira Msemwa na Anjelo Sanga ambao wamepatiwa hati miliki zao kutoka kijiji cha Usungilo wameeleza furaha yao na Kulishukuru shirika la SUMASESU! na serikali Kuwapa Kipaumbele kwenye Mradi Huo wa Upimaji wa ardhi.

"Kwa kweli tunashukuru sana kwa hii fursa kwasababu nina imani makazi yangu yako salama kabisa hata mtu wa kuja kunibughudhi atakuwa hayupo"alisema  Elvira Msemwa 

Christopher Mwamasage ni Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Njombe amesema umiliki wa ardhi wenye hati Ni Utajiri Kuliko kumiliki ardhi bila hati kwani ni sawa na Kumiliki ardhi isiyo na Kitu.

"Tunatoa wito kwa wale wananchi ambao hawajachangia kile kiasi ambacho kinatakiwa waweze kuchangia ili waweze kufanyiwa utaratibu kama huu na waweze kuwa na hati,nimefurahi sana kuwa na ninyi siku ya leo na nimeanzia Makete nafikiri tutaendelea kuwa Makete ili iweze kuwa juu"alisema Christopher Mwamasage 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...