Takriban watu 1,943 wanaarifiwa kuwekwa kizuizini kwenye maandamano yaliyoanza tangu tarehe 20 Septemba nchini Misri.
Wakili wa Misri Halid Ali alitoa taarifa hiyo kwenye akaunti yake ya Facebook na kubainisha kuwa watu wapatao 1,943 wamekamatwa katika maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea tangu Septemba 20 nchini humo.
Ali alisema kuwa takwimu hizo zilizotangazwa na mawakili, zilichulukiwa kutoka kwa jamaa wa karibu wa wahusika pamoja na mashirika ya haki za kibinadamu, kutokana na mamlaka rasmi kukosa kutoa maelezo yoyote.
Ali pia aliongezea kusema kuwa watu hao, walipewa siku 15 za kuwekwa kizuizini na idadi ya watu walioachiliwa huru imeonekana kutowiana na waliokamatwa.
Maandamano dhidi ya serikali yalianza katika maeneo mbalimbali ya nchi mnamo Septemba 20 kufuatia wito wa mkandarasi wa upinzani wa Misri Muhammad Ali anayeishi uhamishoni nchini Uhispania.