Saturday, October 24, 2020

Poshy: Mtoto Wangu Hatokuwa wa Mitandao



JACQULINE Obeid almaarufu Poshy Queen ni mmoja wa warembo ambao wamejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamii, kama Instagram na FaceBook kutokana na umbo lake kuwachanganya wanaume wengi.


Pamoja na umaarufu huo, tayari mrembo huyo amemnasa wake (wa ubani) na muda si mrefu atabarikiwa mtoto na mchumba wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria.


AMANI lilifanya jitihada za kumtafuta Poshy, ambaye amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake huyo ili kujua anaendeleaje na vipi mikakati yake ya harusi na mchumba wake huyo kama ifuatavyo:


Amani: Habari za siku Poshy.


Poshy: Salama vipi Hali?


Amani: Nzuri, umepotea sana na hauna tena mbwembwe kama zamani, kulikoni?


Poshy: Hata nilikuwa sina mbwembwe, basi tu watu walikuwa wakinichukulia tofauti kabisa.


Amani: Hongera mno, nasikia tayari umeshachumbiwa na niliona kwenye media mbalimbali, vipi kwa upande wako kuingia kwenye ndoa hakuna ugumu wowote?


Poshy: Hapana na kwanini nione ugumu wakati mimi ni mwanamke na ninastahili kuwa hivyo, ninachoomba hapa ni kumshukuru Mungu, nikiingia kwenye ndoa niende kuwa mama bora siku zote.


Amani: Nilidhani kwakuwa tayari wewe ni staa na watu wengi kwenye mitandao wanakujua, utasubiri kidogo ndiyo ufikie uamuzi wa kuingia kwenye ndoa?


Poshy: Ndoa ni wewe mwenyewe unavyoipokea na kukubali kuachana na vitu vyote ambavyo siyo muhimu kwenye ndoa yako kama nilivyofanya mimi. Hicho ndiyo muhimu na kwa vile mimi ni mwanamke basi acha nifuate mila na desturi zetu.


Amani: Vipi kwa upande wa mtoto wako, Mungu akikujalia naye unataka awe wa kwenye mitandao?


Poshy: Hapana kabisa, sitaki na nitasimamia hilo, maana mitandao inaweza kupoteza muelekeo wako na kila kitu kabisa.


Amani: Mumeo mtarajiwa sio mtanzania, vipi unaweza kumudu mila za nchi nyingine kama Nigeria ambapo ndiyo asili ya mchumba wako?


Poshy: Hilo halina shida kabisa, kama nyinyi wawili mnasikilizana na kuelewana hilo ndiyo muhimu na si kitu kingine.


Amani: Msomaji wangu angependa kufahamu muda wako wa kulala na kuamka.


Poshy: Kama sina kazi yoyote kwakweli napenda saa tatu niwe nimeshapanda kitandani na kuamka ni mapema mapema sana saa 12 alfajiri niko macho. Amani: Unapoamka unapendelea kunywa chai?


Poshy: Mimi siyo mpenzi wa chai kabisa ila kama nikipata juisi asubuhi nakuwa nimeridhika kabisa.


Amani: Kwa upande wa mlo wa mchana unapendelea kitu gani?


Poshy: Kuhusu mchana  sichagui sana ila napenda chakula kizuri chenye kujenga afya.


Amani: Tuje kwenye upande wa mavazi, mara nyingi unapendelea mitupio gani?


Poshy: Mavazi hayana vitu vingi lakini napenda kuvaa vitu ambavyo vina ubora wa kutosha, kwa mfano nikibeba begi basi liwe la ukweli, ila ninachoshukuru mwili wangu hauhitaji vitu vingi nivaa chochote tu ilimradi kiwe simpo.


Amani: Na gharama unayotumia katika mavazi yako na hata manukato unatumia kiasi gani?


Poshy: Naweza kuvaa nguo ya kawaida tu lakini gharama yake inaanzia 200,000, kuhusiana na pafyumu napendelea za kupoa lakini nzuri kuanzia 300,000 mpaka milioni moja ambayo inaitwa  Mason.


Amani: Watu wengi wana wasiwasi na umbo lako wanadai kuna kitu umefanya, vipi kuhusu hilo?


Poshy: Unajua kila mtu wa pembeni anaweza kuzungumza vyovyote kwasababu hakujui, lakini wanaokujua wananyamaza. Sasa watu kama hao ni kuwaangalia maana kuna wengine wanajifurahisha tu.


Amani: Kutokana na umbo lako unaepukana vipi na usumbufu wa wanaume?


Poshy: Usumbufu upo kwa kila mwanamke ni jinsi tu ya kukabiliana nao na kuongea kistaarabu kwa anayekusumbua basi. Kwasababu mwisho wa siku lazima wewe ni wa mtu maalumu aliyepangwa kwa ajili yako.


Amani: Je kwa sasa biashara zako zinaendaje na duka lako la Poshy Secret bado lipo?


Poshy: Ndiyo na tunaendelea kuuza vitu vizuri vya wadada na kaka zetu wanaojipenda.


Amani: Kwanini uliamua kufungua duka linalouza nguo za ndani na siyo vitu vingine kama nywele na vipodozi mbalimbali?


Poshy: Mimi ninachoamini ni kwamba, hakuna kitu kizuri kwenye mwili kama kuwa na nguo za ndani nadhifu, maana ni fahari na mimi ndivyo napenda nikaona bora nifungue hiki kitu.


Amani: Wanawake wengi wanapenda sana urembo wa nywele lakini wewe uko tofauti na mastaa wa hapa Bongo.


Poshy: Mimi siyo mpenzi sana wa nywele labda itokee tu nivae wigi, napenda sana nywele fupi zilizokatwa Bob Staili.



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...