Wednesday, October 14, 2020

Neymar amkaribia Pele kwa ufungaji wa magoli



Neymar aorodheshwa wa pili nyuma ya Pele katika orodha ya wafungaji bora nchini Brazil kwa kufunga mabao matatu katika michuano ya kuingia kwenye Kombe la Dunia mwaka 2022 dhidi ya Peru.

Mshambuliaji huyo wa kimataiifa wa Paris St-Germain alifunga bao lake la 64 katika mchuano wa kimataifa na kuchagia ushindi wa 4-2.

Peru ilichukua uongozi huko Lima mara mbili lakini Neymar alifunga penalti mbili na kumshinda Ronaldo kwa jumla ya mabao aliofunga huku Pele akiwa na magoli 77.

Neymar, 28, amefunga mabao yake katika michuano 104 ya kimataifa aliyoshiriki huku Pele akiwa amecheza mara 92 kwa ajili ya nchi yake.

Brazil na Argentina iliongoza kundi hilo baada ya kushinda michuano yao yote ya ufunguzi huku Paraguay iliyoishinda Venezuela 1-0 Jumanne, ikiwa ya tatu.

Wanne wanaongoza katika kundi la timu 10 wanafuzu moja kwa moja kwa michuano ya kombe la dunia huko Qatar.



Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...