Tuesday, June 16, 2020

Ugiriki, Israel kushirikiana kwenye utalii na gesi asilia

Ugiriki na Israel zimepanga kushirikiana kwenye kurejea upya kwa shughuli za utalii kati yao katika mwezi Agosti, huku zikieleza wasiwasi wao juu ya hatua ya Uturuki kuanza utafutaji mafuta na gesi kwenye eneo la mashariki mwa Mediterenia.

Waziri Mkuu wa Ugiriki, Ky-ria-kos Mit-so-takis, ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa janga la COVID-19, amefanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, mjini Tel Aviv, kuhusiana na mpango wa nchi zao pamoja na Cyprus kusaka gesi asilia na utalii.

Ugiriki ilifunguwa milango yake jana Jumatatu kwa wasafiri wa Umoja wa Ulaya. Israel, ambayo raia wake milioni 1.2 hutembelea Ugiriki kila mwaka, ni soko kubwa kwa taifa hilo la Ulaya.

 Netanyahu amesema kwamba kuanzia tarehe 1 Agosti, wageni kutoka Ugiriki hawatalazimika kujiweka karantini ya siku 14 kama ilivyo sasa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...