Kuku hupunguza utagaji na hata kuacha kutaga kabisa iwapo:-
Hawakupewa chakula bora au cha kutosha.
Hawapewi maji safi ya kutosha.
Wamebanana, yaani hawakai kwa raha.
Vyombo vya maji au chakula havitoshi.
Mwanga hautoshi.
Majogoo yamezidi katika chumba(weka jogoo 1 kwa mitetea 10)
Kuku wanaumwa.
Wana vidusa vya nje na ndani (external and internal parasite).
Wamezeeka (umri zaidi ya miaka miwili na nusu).
Maumbile ya kuku mwenyewe.