Thursday, May 21, 2020

Palestina yatangaza kusitisha ushirikiano wa kiintelijensia na CIA

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Palestina Saeb Erakat amesema leo kwamba mashirika ya ujasusi ya mamlaka ya Wapalestina yatasitisha hatua ya ushirikiano wa kubadilishana taarifa na shirika la ujasusi la Marekani CIA, kama hatua ya kupinga mipango ya Israel ya kutaka kunyakuwa maeneo ya ardhi yake katika Ukingo wa Magharibi ambayo tokea hapo inakaliwa kwa mabavu na Israel.

Erakat amesema kwamba ni muda wa saa 48 toka walipowaarifu CIA kuhusu hatua yao ya kusitisha makubaliano ya kubadilishana taarifa za kiusalama.

Mamlaka ya Wapalestina ilisitisha mahusiano yote na utawala wa Rais Donald Trump mwaka 2017 ikimshutumu rais huyo kuwa kiongozi anayeupendelea upande mmoja.

Hata hivyo kuna kiasi fulani cha uhusiano usiokuwa wa kisiasa uliobaki ikiwemo uhusiano baina ya mashirika ya usalama ya Palestina na CIA.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...