Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wafanya biashara kutopandisha bei ya bidhaa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani na kuwaagiza wakuu wote wa mikoa kufanya ziara za mara kwa mara kwenye masoko na maduka.
Waziri majaliwa amesema kuwa ameona kupanda kwa bei ya sukari na amewaagiza wafanyabiashara kushusha bei kwani sukari ipo ya kutosha na amewataka wakuu wa mikoa kuwachukulia hatua kari kwa wale ambao hawatashusha bei ya sukari.
" Wiki hii waumini wa kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan hivyo natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu vinauzwa kwa bei ya kawaida, wakuu wa mikoa na wilaya wafanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile" Waziri Majaliwa.
"Hakuna haja ya sukari kupanda kuliko ile bai yake ya kawaida…bei itaendelea kuwa ile ile…ninawaagiza wakuu wa mikoa yeyote…atakayeuza kilo kwa shilingi 4500 chukua hatua kali dhidi yake" - Waziri Mkuu