Friday, April 10, 2020

Tukumbushane haya yaliyo ya muhimu katika maisha

Sisi binadamu kwa namna moja ama nyingine tunatakiwa tuishi kama ndugu kwa kuelimishana na kukumbushana yale yaliyo ya muhimu yatakayotujenga katika maisha yetu kama ifuatavyo;

Punguza
Ukitaka kuachana na inzi tupa kwanza mzoga ulionao, namaanishaa ukitaka mafanikio punguza kwanza marafiki hewa, wanafiki na watu wasiyona maana kwenye maisha yako.

Kumbuka.
Usaliti siyo bahati mbaya, ni makusudi. Kumpa nafasi ya pili msaliti ni kujitesa mwenyewe.

Nakuambia kweli..
Ukihisi wanakusema na ukahamaki kwa hasira ujue hujiamini ila ukiona wanakusema na ukawapuuza ujue unaakili.

Nakusisitiza.
Mheshimu mjinga uokoe muda na kuepukana na shari au balaa.

Naongea na vijana wenzangu.
Acha akili za kicheche kila saa wewe kufikiria mapenzi tu, think deeper fanya mambo yenye malengo kwenye maisha yako.

Naongea na wadada.
Facebook siyo dampo la kupost picha zako zisizo na maana, uheshimu na kuusitiri mwili wako, wanaume tunataka mtu anaye jiheshimu siyo mtu anayetupa presha mitandaoni

Utafanikiwa.
Acha ujuaji (much know) hakuna anayejua kila kitu hapa duniani, sikiliza ushauri ufanikiwe.

Sikiliza mama yangu.
Familia haijengwi kwa umbea wa mtaani, shirikiana na mumeo utaijenga familia bora na imara.

Sikiliza kaka yangu.
Mke mzuri atafutwi messanger, instagram wala kwenye group la whatsap, mke mzuri anapatikana kwa kumshirikisha mungu siyo kwa matamanio ya macho.

Acha dharau.
Kufika mbili kunaitaji kuanza moja stage after stage, kamwe huwezi toka stage moja kwenda nyingine kama una chuki, dharau wala kujiona daima utabaki mkia tu.

Nina uhakika.
Hofu na woga ndiyo chanzo cha kurudi nyuma kimaendeleo, punguza hofu.

Halipingiki.
Kumpenda asiye kupenda ni sawa na kutegemea jasho kwenye ulimi, na kumsahau uliye mpenda ni sawa na kumkumbuka usiye mjua.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...